Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Kiplimo Lelei ametoa wito wa ushirikiano baina ya walimu na wanafunzi kama njia moja ya kupata ufanisi masomoni.
Akihubiri katika Misa kwenye shule ya upili ya wavulana ya St Peters Marakwet alitoa wito kwa wanafunzi hao kumshirikisha mwenyezi Mungu ambaye anasema ndiye atawajalia ujasiri.
Aliwashukuru wazazi kwa bidii Ya kujinyima kwa lengo la kufanikisha masomo ya wanao.
Aliwataka wazazi pamoja na walimu kuwapa wanafunzi hao motisha akiwaonya wanafunzi dhidi ya kushiriki udanganyifu katika mitihani ya kitaifa akisema kuwa njia za mkato ni haramu na madhara yake hairidhishi.