Askofu msaidizi John Kiplimo Lelei ametoa wito kwa vijana nchini almaarufu Gen z kuwa na Subira Kila wanapotoa shinikizo yao.
Askofu Lelei alisema kuwa, ingawa washinikiza maswala muhimu nchini kadhalika, wanstahili kuwapa sikio viongozi na kuwa na Subira ili maswala wanayoshinikiza iweze kutatulia.
Alitoa wito kwa vijana kumpa rais William Ruto Muda wa kutekeleza hayo kwa kuwa rais tayari ameonyesha nia ya kutekeleza hayo.
Haya yanajiri baada ya rais William Ruto kufutilia mbali Baraza lake la mawaziri na Kutia sahihi mswada wa tume ya IEBC.