Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria amewataka wazazi kuwaelekeza wanao kwa upendo japo wanaweza kuwa wamekosea.
Akihubiri wakati wa hafla ya Famly day katika kathedrali ya St.Paul and Peter katika jimbo la Embu,amesisitiza umuhimu wa subra miongoni mwa wazazi kama njia moja ya kuwanusuru wanao kutokana na uraibu wa dawa za kulevya.
Askofu mkuu alisema kwamba wazazi wanapaswa kuwa wenye moyo wa msamaha kwa wanao ndipo waweze kuasi hulka zisizostahili.
Wakati huo,askofu mkuu aliwataka wakristu kuwa wakarimu kwa kila mmoja pasi na ubaguzi wowote kulingana na mafundisho yake kristu.