ARCH SUBIRA:Sala nguzo kwa mkristu

Wakristu wametakiwa kuwa na hulka ya kusali kila wakati kwa kuwa sala humleta mwenyezi Mungu karibu na mja wake.

Akihubiri katika misa ya kipaimara kwenye kanisa la mtakatifu  Yosefu Mukasa Kahawa West, askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Subira Anyolo alisema kuwa kujisadaka bila kujibakisha katika sala hupyaisha maisha ya binadamu na humkinga dhidi ya maovu ambao kwa sasa yamekithiri ulimwenguni kote.

Alisema kuwa misukosuko nyingi katika familia inawezakutolewa tu kwa njia ya sala akitoa wito kwa kila familia kujikita katika sala kila wakati bali sio wakati wa majanga pekee.

Kadhalika askofu mkuu alitoa wito kwa wakristu kujitahudi kupokea sakramenti ya kipaimara akisema kuwa hii ni sakramenti ambayo mkristu humkaribisha kwa nafasi ya kwanza roho mtakatifu ambayo ni mungu katika nafsi ya tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *