Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka amepuuzilia mbali baraza jipya lililoteuliwa na rais William Ruto akisema kuwa rais angeteua sura mpya katika baraza hilo.
Akizungumza na wanahabari Askofu Oseso alisema kuwa kule kuwarejesha wale waliohudumua katika baraza hilo ni kukejeli wakenya ambao wamekuwa na matarajio makubwa katika baraza hilo, akitoa wito kwa wabunge watakaowapiga msasa kuwaweka pembeni.
Alisema kuwa uteuzi wa mawaziri wa hapo awali katika baraza jipya ni dhihirisho kuwa rais hajasikiliza sauti ya wakenya walioandamana wakishinikiza mageuzi nchini.