Ipo haja ya wazazi kutangamana na watoto wao kama njia moja ya kutatua changamoto zao wakati wa likizo wa muhula wa pili.
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Lelei amesema kuwa huu ni wakati wa wazazi kuwasilikiza wanao na kurekebisha changamoto zao akisema kuwa mzazi ana nafasi ya kwanza katika swala la malezi kwa kuwa hulka ya kuwatelekeza wanao huenda ikaathiri kwa kiwango kikubwa kizazi kijacho.
Ametaja mtandao kama donda sugu katika swala la malezi akihimiza kila mzazi kuwa mwangalifu zaidi akisema kuwa majukwaa mbalimbali kwenye mitandao yamepalilia hulka mbaya miongoni mwa vijana jambo ambalo limechangia visa vingi vya utovu wa nidhamu.
Askofu lelei amewataka wazazi kuzungumza na kizazi cha sasa che Gen z na kuwaelekeza vyema akisema kuwa wanarika hao wako katika hatari ya kupotoka kitabia iwapo wataachiliwa mikononi mwa wenzao na mitandao ya kijamii, akitaka kila mzazi kuchukua jukumu la kuziba kila pendo kwenye malezi kwa faida ya kizazi kijacho.