Magenge yachipuka kwenye serikali za kaunti

Hali ya wasi wasi mjini Kpasabet kaunti ya Nandi ambapo vijana waliojihami kwa rungu walikusanyika mapema leo kukomesha maandamano dhidi ya gavana wa kaunti hiyo Stephen Sang.

Vijana hao waliokuwa wamekita kambi katika kituo cha Namgoi kando ya barabara ya kuelekea Eldoret ambako waandamanaji walikuwa wameratibu misururu ya maandamano,wakaazi wakiwemo aliyekuwa mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter  wamekuwa wakiandaa maandamano hayo lengo likiwa ni kumwajibisha gavana Sang.

Hata hivyo gavana Sang akijibu tukio hilo la vijana kujihami amesema kuwa vijana hao wanalengo la kuwalinda wafanyibiashara mjini humo dhidi ya uporaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *