Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivua Musonde amesema kuwa vita vita vinavyoshuhudiwa kwa Sasa katika mataifa mbalimbali vimechochewa ni uongozi mbaya.
Akirejelea Hali ilivyo kwa Sasa nchini Haiti askofu mkuu Kivuva alisema kuwa taifa hilo limetumbukia kwenye Lindi la machafuko kutokana na ukosefu wa Nia nzuri kutoka kwa viongozi na sera Bora akitahadharisha mataifa mataifa ambayo yametekwa nyara na ufisadi kuwa huenda yakajipata pabaya.
Kadhalika alitoa wito Kwa viongozi kutelekeza wajibu wao kwa umoja pasi na kunyosheana kidole cha lawama kwa faida ya mshikamano wa wananchi.