Mua Hauliki

Wakulima wa miwa katika maeneo ya Maraba na Kameloi eneo bunge la Aldai kaunti ya Nandi wameandamana kulalamikia kusitishwa kwa ujenzi wa barabara ya Kipkorok kuelekea miwani ,uliokua unafanywa na kampuni moja ya kusaga unga.

Kampuni hiyo ilisitisha ujenzi huo,kwa kuhofia mapendekezo ya mswada wa sukari,unaopendekezwa kutengwa kwa maeneo ya wakulima kupanda miwa.

Sasa wakulima hao wanataka kilio chao kisikizwe na serikali ili waweze  kuendelea na shughuli zao za ukulima,wakidokeza kwamba wanapitia hali ngumu kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *