Jitume ughaibuni

Katibu katika wizara ya leba na ulinzi wa kijamii Shadrack Mwadime amewataka wakenya ambao wamepata fursa ya kusafiri katika mataifa za ughaibuni kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo ipasavyo.

Akiongea na wanahabari katika kaunti ya Uasin Gishu,katibu huyo anasema taifa imeongeza kiwango chake cha mapato kupitia wananchi hao, ambao wanaendelea na shughuli zao katika mataifa mbalimbali ulimwenguni akieleza kuwa ni hatua nzuri hilo.

Hata hivyo,kuhusiana na baadhi ya wakenya kuteseka kwenye baadhi ya mataifa hasa zile za milki za kiarabu,Mwadime amewataka wakenya kuhakikisha kwamba, wanapitia mawakala walioidhinishwa kuepuka wao kujipata katika hali hiyo.

Aidha,amesema wameweka mipango ya kuwahusisha makampuni na wakala mbalimbali wanaowasafirisha wakenya kwenda mataifa za nje, kutafuta ajira ili kuwaweka salama wananchi hao na wao pia kupata ajira.

Yanajiri haya,wakati na ambapo hapo awali wakenya wengi ambao walisafiri kwenye mataifa za ughaibuni kutafuta ajira, walijipata kwenye mikono ya waajiri waliowadhulumu hata wengine wakipoteza maisha,huku baadhi yao wakilaghaiwa pesa zao na baadhi ya mawakala wa makampuni ya kusafirisha wakenya nje ya  nchi kupata ajira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *