Biashara kiimarike uchumi ikue

Kamati ya biashara,viwanda na mashirika katika bunge la kitaifa limeendelea kukusanya maoni kutoka kwa wafanyibiashara na wakaazi katika maeneo mbalimbali nchini, kutathmini masuala ambayo yanapaswa kujumuishwa kwenye mswada unaolenga kupitishwa la kuwalinda wafanyibiashara nchini.

Wakiongozwa na naibu mwenyekiti wao ambaye ni mbunge wa Teso Kusini Otuoch Mary Emaase,ni kuwa wanaendelea na kukusanya maoni hayo kutoka kwa wananchi kupitia mikutano zinazoandaliwa katika kaunti zote 47.

Wakizungumza mjini Eldoret,viongozi hao walisema ipo haja ya kuweka sheria ambayo wafanyibiashara watajikatia leseni ambayo itawasaidia kugharamika mara moja tu wakati wanaendelea na biashara zao,suala lililochochea ni kwa wafanyibiashara wanapozuru kaunti zingine wanalazimika kulipia mara dufu na kuwapa hasara kwenye biashara zao.

Wakati huo,kamati hiyo inasema kwamba hatua hii itasaidia kuimarisha ushirikiano wa serikali za kaunti na ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *