Mbunge wa Chesumei kaunti ya Nandi Paul Biego amezitaka idara husika zinazoendeleza uchunguzi kuhusiana na mbolea bandia kuharakisha uchunguzi huo na watapeli kwenye sakata hiyo kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa soko la kisasa katika eneo la Mosoriot kaunti hiyo,mbunge huyo alisema kwamba, usambazaji wa mbolea ghushi inawatia kiwewe wakulima na kilimo itakua kwenye hatari na iwapo swala lenyewe halitashughulikiwa mara moja, huenda uzalishaji wa chakula nchini ikaathirika na kusababisha njaa sikuza baadae nchini.
Kadhalika,mbunge huyo ametaja usambazaji wa mbolea katika kituo cha Mosoriot umekuwa wa kuridhisha akisema mbolea kutoka kwa serikali ni halali.