Shule tano za msingi katika kaunti ya Baringo zimefungwa kufuatia makabiliano makali kati ya wenyeji na wezi wa mifugo kwa muda wa wiki mbili.
Shule hizo zinazojumuisha Kosile, Ngaturo, Kibenos, Kagir na Iata zimefungwa kutokana na misururu ya mashambulizi katika eneo hilo ambayo yamepelekea vifo vya watu wawili wakiwemo mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kagir Thomas Kibet.
Viongozi katika eneo hilo sasa walitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati wakisema kuwa hali ilivyo kwa sasa katika eneo hilo wakisema kuwa watu wanane tayari wamepoteza maisha yao katika eneo hilo kufuatia mashambulizi hayo.