Kilimo uti wa mgongo

Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei ametoa wito kwa serikali kuu kuweka mbinu mwafaka wa kuhakikisha kuwa mbolea ya ruzuku inawafikia wakulima wote katika ameneo ya mashinani kama njia moja ya kuafikia utoshelezo wa chakula nchini.

Akizungumza katika eneo bunge la Mosop kaunti ya Nandi seneta huyo alisema kuwa itakuwa vyema kwa wizara ya kilimo kuhakikisha kuwa mbolea hiyo inawafikia wakulima walio katika maeneo ya mashinani ambao anasema kuwa wanagharamika zaidi kusafiri ili kutafuta bidhaa hiyo.

Kuhusu mswada wa ushuru wa nyumba za bei nafuu seneta huyo amehaidi kuwa bunge la seneti litapitisha mswadu huo bila ya kuifanyia marekebisho.

Macho yote sasa yameelekezwa katika bunge la seneti baada ya lile la kitaifa kuupitisha mswada huo mapema juma hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *