kilimo biashara mambo yote

Wakaazi kaunti ya Uasin Gishu wameshauriwa kuhakikisha wanajishughulisha na kilimo biashara ili waweze kujikimu na kujikwamua kutokana na hali ngumu ya maisha.

Akizungumza katika eneo la Kapseret,gavana wa kaunti hii ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amesisitiza haja ya wakulima kuwa wabunifu na kuwaacha kutegemea mfumo wa zamani wa kupanda zao moja ya chakula akieleza serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia.

Amesema kwamba kuna kiwanda tayari ambayo serikali kupitia washirika kujenga kiwanda cha parachichi ndipo wakulima wa zao hilo na waweze kupata manufaa kupitia zao hilo.

Wakati huo amesema serikali ya kaunti imeweka mikakati ya kusaidia wakulima kwa ukulima wao kupitia kilimo cha unyunyuziaji akisema kwamba tayari kuna vifaa hitajika kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *