Wanafunzi zaidi ya Elfu arobaini na nane katika kaunti ya Pokot Magharibi hawaendelei na masomo yao ya shule za upili na vyuo vikuu kutokana na ukosefu wa karo.
Akizungumza mjini Kapenguria,Gavana wa kaunti hiyo Simon Kachapin alisema kwamba wanafunzi hao wameshindwa kuendelea na masomo yao kwa kuwa wengi wa wakulima wanafuga mifugo ambao ukame ukiwadia mifugo wengi hufa na kuchangia umaskini kwenye familia hizo.
Kachapin hata hivyo alisema serikali ya kaunti hiyo imeweka mikakati ya kuwasaidia wanafunzi hao ili kuwainua kimaisha.