Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde ametoa wito kwa wakristu kutolaghaiwa na manabii wa uongo ambao kwa sasa wantumia dini kuwapotosha waumini.
Akihubiri katika misa ya daraja la upadirisho wa mashemasi wawili eneo la Bura jimbo kuu katoliki na Mombasa askofu Kivuva ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa katoliki nchini KCCB ametoa wito kwa kila mmoja kutekeleza wajibu wa kisimama kidete kupitia sala na utiifu akisema kuwa huo ndio utakaoweka msingi dhabiti wa imani.
Askofu kivuva kadhalika amewataka wakristu kutumia kipindi hiki cha mfungo wa kwaresima kuwahubiria habari njema walioteleza kwa kuwaonyesha na kuwatendea matendo mema.