Mfungo wa siku arobaini kwa kalenda ya kanisa katoliki ukiwa umengo’a nanga kwa jumatano ya majivu na kilele chake kikiwa pasaka,maskofu wa jimbo katoliki mbalimbali nchini wamewataka waumini kuwa mstari wa mbele kurejesha imani yao kwa kristu kwa kutubu dhambi zao.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira ametoa wito kwa wakristu kuwa tayari kukiri dhambi zao na kuwaweza kusonga karibu na mwenyezi mungu.
Askofu mkuu anyolo ametoa wito kwa serikali kuimarisha kampeni zake za kupambana na Ufisadi.
Kauli ambayo imeungwa mkono na askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ambaye amesema sharti swala la ufisadi likomeshwe nchini kwa taifa la bwana lililo na mwelekeo.
Askofu Norman King’oo Wambua ni askofu wa jimbo katoliki la Machakos na ujumbe wake ni huu.