Jinyime kutafakari mafumbo ya Kwaresima

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka wakristu wote wa jimbo kutumia kipindi cha kwaresima kutafakari kusali na kufanya matendo ya kiutu.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret DomINIC Kimengich amesema kuwa huu ni wakati wa kutafakari namna ya kupambana na maadui watatu ukiwemo ukabila, ufisadi na kujikita katika sala na sakramenti ya toba ambayo anasema kuwa ni agano kati ya muumba ni mja wake.

Kadhalika askofu amewataka waumini kujitwika jukumu la kufanya matendo ya kiutu akisema kuwa huu ni wakati wa kujinyima kutokana na matendo mbalimbali ambayo wakristu wamezoea kama njia moja ya kutafakari safari ya wokovu.

Ametoa wito kwa wakristu kadhalika kujiepusha na ukabila ambayo anasema ndio chanzo cha ufisadi nchini ambayo hupelekea wananchi wengi kukosa rasilimali mashinani, na kutokana na ukosefu huo katia maeneo ya mashinani husababisha migogoro miongoni mwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *