Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka ametoa wito kwa wakristu kujiepusha na hulka ya kulipisha kisasi akisema kuwa hulka hiyo haidhihirishi upendo wa mkristu kwa mwenyezi Mungu.
Akihubiri katika misa iliyowaleta pamoja waumini wa jimbo katoliki la Nakuru wanaofanya Kazi jijini Nairobi , askofu Oseso Tuka alisema kuwa kipindi cha kwaresima huwapa wakristu nafasi ya kutambua nguvu iliyopo kwenye msamaha, akikanya wale walio na hulka ya kulipisha kisasi kukumbatia msamaha.
Askofu huyo alisema kuwa njia moja tu ya kuwabadilisha wale wanaowatendea maovu sio kwa kulipisha kisasi bali kuwatendea mema na siku zote kuwaweka katika sala na kuwabariki kwa kuwa kristu ana nguvu ya kubadilisha hata yale yaliyofichika.
Alitoa wito kwa wakristu kutafakari kipindi hiki cha kwaresima kwa kujirudia na kujiepusha na mambo ya kawaida na badala yake watekeleza yale yaliyo haki na kushiriki sakramenti ya toba