Komesheni siasa ama kiwarambe

Wito umetolewa na kwa viongozi wa kisiasa nchini kuimarisha nguvu zao kuwahudumia wakenya badala ya kuanza kurindima ngoma za siasa.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria katika ujumbe wake siku ya Jumapili ametoa wito kwa viongozi wote waliochaguliwa kukoma kurindima ngoma za siasa na badala yake watekeleze ambayo waliahidi wakenya kuelekea uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka wa 2022.

Askofu Muheria kadhalika ametoa wito kwa viongozi wa upinzani na wale wa serikali kushiriki mazungumzo kama njia moja ya kutatua maswala kadhaa ambayo kwa sasa imewasakama wakenya ikiwemo hali ya juu ya gharama ya maisha.

Ametoa witjo kwa viongozi wa kidini kuongoza kwa vitendo kwenye harakati ya kutafuta suluhu kwa changamoto inayowakera wakenya nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *