Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amewataka wanariadha nchini kupata ushauri zaidi wa namna ya kutumia fedha kama njia moja ya kuzuia maafa yanashuhudiwa kwa sasa kutoka kwa wale walio na nia ya kuwatapeli.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya mbio za nyika alamarufu Sirikwa classic Cross Country gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim alisema kuwa ukosefu wa elimu bora katika maswala ya kifedha, ndio imechangia wanariadha wengi kupoteza maisha yao mikononi mwa matapeli.
Gavana bii kadhalika aliwarai wanariadha nchini kuwa makini na kujiepusha mamatumizi ya dawa za kusisimua misuli ambayo alisema kuwa imekuwa kero kwa wanariadha wengi na hata kudidimiza matumaini yao ya kung’aa katika ulingo huo.
Naye rais wa shirikisho la riadha nchini Jackson Tuwei alitoa wito kwa idara husika ikiwemo ile ya michezo pamoja na mazingira kuhakikisha kuwa kambi za wanaridha na hata nyuga zao zisalie safi kama njia moja ya kuwaweka wanariadha salama kiafya.