Askofu mkuu wa kanisa la kiangilkana nchini Jackson Ole Sapit ametoa wito kwa wabunge kutupilia mbali miswada ambayo huenda ikawakandamiza wakulima nchini.
Akiongea na wanahabari mjini Eldoret askofu mkuu huyo aliwataka wabunge kutupilia mbali mswada unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni ya kutoza ushuru mazao ya wakulima akisema kuwa ni sheria ambayo itamkandamiza mkulima akitaka wakenya kutoa sauti kwa kauli moja kupinga mswada huo.
Kadhalika alitoa wito kwa viongozi katika vitengo vyote vya serikali kushirikiana pasi na kuwa na malimbano baina yao akisema kuwa malumbano yanayoshuhudiwa kwa sasa yatadidimiza maendeleo ya taifa.