Wito umetolewa kwa asasi zote za serikali kuimarisha doria katika eneo la bonde la kerio kwa kukabiliana na majangili hao bila mapendeleo.
Kiongozi wa kanisa la Kiangilkana nchini askofu mkuu Jackson Ole Sapit alitoa wito kwa asasi za kiusalama kuimarisha doria katika eneo la bonde la Kerio bila kuegemea kabila, akitoa wito kwa idara hizo kuhakikisha kuwa hali ya utulivu inarejea.
Sapit kadhalika aliwataka jamii zinazoishi katika maeneo ya mpakani kukumbatia amani na kuhubiri amani katika eno hilo kama njia moja ya kufanikisha mshikamano wa kijamii.
Kuhusu mauji dhidi ya kinadada ambayo kwa sasa yanashuhudiwa hivi sasa kiongozi huyo alitoa wito kwa idara ya makosa ya jinai kufanya uchunguzi wa kina akitaka kila mkenya kujiadhara na wale wanaotangamana nao.