Mwanaharakati mmoja wa haki za kibinadamu katika kaunti ya Uasin Gishu anasema kwamba maisha yake yamo hatarini baada yake kudai kupewa vitisho na kundi la vijana hii ikihusiana na kazi yake ambayo amekua akitekeleza katika kaunti ya kutetea haki za kibindamu.
Afisa huyo Kimutai Kirui alidai kwamba kundi hilo linamtishia maisha na kumuonya vikali dhidi ya kutoa matamshi ya kukashifu serikali ya kaunti ya Uasin Gishu.
Mwanaharakati huyo akizungumza mjini Eldoret alisema kwamba tayari ameandikisha taarifa na polisi kuhusu vitisho hivyo huku akiapa kuendelea na shughuli zake za kuwatetea wanyonge katika jamii bila uoga wowote.