Shirikianeni katika kukuza shamba la bwana

makleri na majandokasisi wametakiwa kushirikiana na wakristu kwa sala na toba  kama njia moja ya kukabiliana na mawimbi ya maisha.

Akihubiri katika misa ya family day Jimbo katoliki la Kisii askofu wa jimbo hilo Joseph Mairura Okemwa amewataka watumishi wote katika shamba la bwana kutohofu kushambuliwa na wale ambao hawajasadiki kristu katika utendakazi wao akihoji kuwa hakuna wito bila changamoto zake.

Askofu huo kadhalika amewataka makleri kuwa radhi siku zote kuwahudumia wakristu kwa upendo wakiwapokea katika njia salama na kuwaonyesha ramani ya kwenda mbinguni.

Amehaidi kuwajengea mapadre jumba la wazee na zahanati ambayo itasaidia kuwasitiri mapadre wakongwe na hata kuhudumia wakati ambapo kutakuwa na hitaji la huduma ya kiafya.

Askofu kadhalika amewatakia uponyaji wa haraka wakristu na wakenya wote ambao kwa sasa wanaugua maradhi mbalimbali kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *