pokeeni njia mbadala ya kutatua kesi [AJS]

Viongozi mbalimbali katika kaunti ya Uasin Gishu wakiwemo viongozi wa kidini na wazee wa mitaa wanaendelea kupokea mafunzo  kuhusu namna ya kutatua mizozo miongoni wa watu wanaoishi nao kwa kutumia njia mbadala

Mkurugenzi wa shirika la North Rift Theatre ambassadors ( Norta) Ken Ruto akizungumza kwenye mkutano wa uhamasisho mjini Eldoret alisema wamechukua jukumu hilo ili kuwawezesha kujua jinsi ya kutatua mizozo kwa njia ya upatanisho akiongeza kwamba wataelimisha  jamii kwa ujumla kuhusu namna ya kutafuta haki kwa njia mbadala kwenye kesi mbalimbali zikiwemo zile za mzozo wa urithi.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wamesema kwamba wamejifunza namna ya kutafuta haki baada ya kupokea mafunzo hayo.

Aidha baadhi ya wazee wa mitaa katika kaunti hiyo wanasema kwamba jamii imeanza kukumbatia njia mbadala ya kutafuta haki na kuongeza kwamba wazee wameweza kushughulikia kesi nyingi zikiwemo zile za mizozo ya ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *