mwanapatholojia atakiwa mahakamani

Mahakama mjini Eldoret imemwamuru mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor kufika mahakamani ili kujibu maswali kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanamtindo Edwin Kipruto almaarufu Chiloba.

Jaji Reuben Nyakundi ameagiza mwanapatholojia huyo kufika ili kutoa ripoti za upasuaji uliofanyiwa mwili wa Chiloba na habari zilizopelekea kifo cha mwanamtindo huyo wa ndoa za jinsia moja alamarufu LGBTQ.

Kuamriwa kwa mwanapotholojia huyo kufika mahakamani ilitokana na ombi la wakili wa serikali Mark Mugun kuwasilisha ombi mahakamani la kutaka matokeo ya upasuaji wa mwili wa mwanaharakati Chiloba kuwasilishwa ili kubaini kilichopelekea kifo chake.   

Hata hivyo mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanaharakati huyo Jacktone Odhiambo atasusubiri hadi ijumaa juma hili, ili kubaini iwapo ataachiliwa  kwa dhamana au la.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *