Jamii katika kaunti ya Nandi imetakiwa kuwa msitari wa mbele katika vita dhidi ya dhulma za kijinsia ambavyo vimeongezeka katika siku za hivi karibuni.
Wanaharakati wa jamii na viongozi mbalimbali wanasema kuwa wakati umewadia kwa kila mmoja kuzungumzia dhuluma za kijinsia, ambapo wanawake na wasichana wadogo wanaendelea kunyanyaswa.
Haya yanajiri kwenye hafla ya kumkumbuka mwanariadha Agnes Tirop kutoka Nandi aliyeuawa kinyama kutokana na tofauti za kifamilia na mpenziwe miaka mitatu iliyopita.