Wanafunzi wa darasa la nane waliopokea matokeo yao mwaka huu wakitarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wazee wa mitaa na machifu wametakiwa kumakinikia zoezi hilo ili kuafikia asilimia mia.
Kamisna katika kaunti ya Uasin Gishu Edyson Nyale aliwataka machifu manaibu wao pamoja na wazee wa nyumba kumi kushirikiana pamoja na wazazi ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanajiunga na kidato cha kwanza kama ilivyoagizwa na serikali.
Naye naibu gavana wa kaunti hii John barorot aliwataka wazazi kuangazia swala la elimu kwa usawa bila kutelekeza jinsia moja na kupendelea jinsia nyingine.
Kamishna Edison Nyale kadhalika aliwataka vijana wote kujiadhari haswa wakati huu ambapo taifa linashuhudia mvua kubwa ili wasije wakaangamia.