Tumieni wito wenu kuwaelekeza wengine

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka makatekista kutumia wito wao kuwaelekeza wato katika njia ya wokovu.


Akihubiri katika Misa ya kusherehekea mtakatifu Charles Boromeo katika uwanja upadirisho wa kanisa la moyo mtakatifu wa Yesu kathedrali askofu amewataka makatekista kuiga mfano wa msimamizi wao aliyejisadaka bila kujibakisha katika utendakazi wake kuelekea wokovu.


Askofu kadhalika amewataka makatekista kuw mfano Bora kwa kusihi maisha ya sakramenti ili iwe rahisi kwao kuwaelekeza watu katika sakramenti akisema kuwa makatekista ndio barua inasomwa na wakristu.


Ametoa wito wa ushirikiano kati ya makatekista hao na mapadre kama njia moja ya kufanikisha ruwaza ya jimbo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *