USAJILI WA CHAMA UDA

Wakaazi wa kaunti ya Uasin gishu wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujisajili na hata kuwania nyadhifa mbalimbali za mashinani katika uchaguzi wa chama cha UDA ambao umeratibiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa chama hicho katika eneo la Kati Peter Mbogo ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti hii ya Uasin gishu kujitokeza na kujisajili kama mwanachama wa chama hicho akisema kuwa chama hicho tawala kimejitolea kikamilifu ili kuhakikisha kuwa huduma zote zinawafikia wananchi kama ilivyohaidi kuelekea uchaguzi mkuu uliopita.

Viongozi hao kadhalika waliwahakikishia wenyeji kuwa kutakuwa na usawa na zeozi hilo litakuwa wa kidemokrasia wakitoa wito kwa wanachama wa zamani kukumbatia na kuwakaribisha wanachama wapya ambao watataka kuwania nyadhifa mbalimbali……

Haya yanajiri baada ya chama hicho tawala kutangaza kuandaa uchaguzi mwezi wa Disemba tarehe tisa Akitoa wito kwa wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali kuwasilisha makaratasi yao kabla ya tarehe mbili mwezi wa November.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *