Kumbukumbu ya sita ya Bishop Korir

Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa hafla ya kumbukumbu ya sita ya askofu wa tatu wa jimbo hilo Cornelius Korir aliyefariki dunia yapatao miaka sita zilizopita.

akiongoza misa hiyo askofu wa jimbo hilo Dominic Kimengich amemtaja mtangulizi wake kama jasiri wa imani aliyejisadaka bila kujibakiza akitoa wito kwa wakristu wote wa jimbo hilo kuiga mfano wake kwa kusimama kidete katika maswala ya imani.

Askofu Kimengich kadhalika amehaidi kufuata nyayo za askofu Korir za kuleta uwiano na utangamano miongoni mwa jamii zinazozozana katika eneo la bonde la Kerio.

amesema kuwa jengo kubwa la St Johns Amani centre linalojengwa katika kanisa la Moyo mtakatifu wa Yesu Kathedrali alikozikwa askofu Korir ni kwa heshima ya askofu Korir aliyejulikana kama balozi wa imani kutokana na juhudi zake za kuleta amani.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *