Hakimu kwenye mahakama ya Eldoret ya kutatua mizozo madogomadogo Tabitha Wanjiku amesema kwamba japo ujio wa mahakama hizo zitakuwa za manufaa kwa wakenya,kwa sasa uhaba wa mahakimu unaweza kulemaza juhudi za kutatua kesi za waathirwa kwa muda mwafaka.
Akizungumza mjini Eldoret baada ya kuapishwa kwa mahakimu hao watatu hiyo jana na jaji wa mahakama ya Eldoret Rueben Nyakundi,hakimu Wanjiku amesema kwa mpangilio uilopo kwenye Mahakam hizo ndogo ni kwamba waathiriwa wanapowasilisha kesi zao,kesi hizo zastahili kutatuliwa kwa siku sitini swala analosema ni changamoto iwapo kesi nyingi kwa uhaba wa mahakimu hao.
Hakimu huyo kadhalika anaeleza ni kesi zipi ambazo mahakama ya small Courts Claim hutatua akisema kwamba wanatatua maswala ya kibiashara,kesi hizi zikianza kuanzia shillingi 1,000.