Taifa litasimama imara kwa mwongozo bora

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira ameweka wazi kwamba kanisa halitafumbia macho ukiukaji na utumizi mbaya wa rasilimali ya umma na itasimama imara kulielekeza serikali inapostahili.

Akizungumza katika shule ya Mtakatifu Maria Msongari wakati wa hafla ya Family Day ya dekania za Kabete na Central,askofu Anyolo amesema kwamba uongozi bora ni ule unakubali kuelekezwa na kanisa kwa kuwa inawakilisha wakenya wnegi wasiokuwa na sauti itasimama imara kuongea kwa niaba yao kuielekeza serikali ili kila mmoja aweze kufurahia matunda ya uchaguzi na vilevile maendeleo kwao.

Askofu Anyolo vilevile aliwashauri wenyeji kuwa makini na maamuzi yao ikizingatiwa kwamba uchaguzi ulikwisha kamilika ila watakapo pewa fursa tena kuwachagua viongozi wawe na uamuzi wa busara ambapo hawatalalamika na iwapo watawachagua viongozi wao wakue tayari kuwapokea na kuwapa nafasi ya kutekeleza yale wanazohitaji bila ya kunungunika.

Aidha,aliwataka wakenya kuendelea kuliombea taifa hili lijikwamue kwenye lindi la kudorora kwa uchumi kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha akiwataka wakenya kushirikiana ili kuafikia maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *