IMARISHENI IMANI YENU

Wito umetolewa kwa wakristu kusimama imara kiimani kwa kuwa tayari kutubu dhambi zao.

Akihubiri wakati wa hafla ya upadrisho kwa mashemasi katika dyosisi ya Kisii,askofu wa jimbo hilo Joseph Mairura Okwemo amewataka wakristu kutambua kwamba katika ulimwengu huu uliojaa maswala mengi,hakuna mwanadamu mtimilifu na kwa hilo wanaweza kuwakosea wengeni na kwa hilo wanastahili kuomba msamaha.

Amewataka pia makleri na majandokasisi kuwa mstari wa mbele kuwaonyeshi njia salama waumini na kujitenga na mambo yale ambayo huenda yakawapotosha na kusahau miito walizotunukiwa za kuwa viongozi na kuwajengea imani wakristu.

Askofu OKwemo vilevile amewataka watumishi katika shamba la bwana kuheshimu wito wao kwa kuzingatia utendakazi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *