Bidhaa zakamatwa

Maafisa wa polisi kaunti ya Uasin Gishu wamenasa bidhaa ya nyumbani ya kielektroniki katika duka moja hapa mjini Eldoret.

Akithibitisha haya kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi amesema kwamba maafisa wa polisi walinasa bishaa hizo kwa duka ambayo kwa mujibu wa leseni yake hastahili kuziuza.

Amesema kwamba walipata bishaa kama vile aina tofauti ya rununu yapatayo 156,tarakilishi  33 mitungi ya gesi 27 miongoni mwa bidhaa nyinginezo.

Mwanthi hata hivyo amewataka wakaazi kujiepusha na biashara isiyostahili na kuhakikisha kwamba wanazingatia maelewano yao ya kibiashara huku akiwataka kufika kwenye kituo cha polisi cha Central Eldoret kubaini iwapo bidhaa zao zilizopota zipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *