KCCB:Tembeeni kisinodi

Mkutano mkuu wa Sinodi ukielekea ukingoni juma hili,wakristu wametakiwa kutembea pamoja na kusikiliza sauti ya kila mmoja kama inavyonogeshwa kwenye Sinodi.

Akiongea katika kanisa la Mtakatifu Peter mjini Vatican wawakilishi wa baraza la maaskafu wa katoliki nchini KCCB wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Martin Kivuva Musonde amesema kuwa jamii hapa nchini inastahili kuiga ruwaza ya sinodi hiyo kwa kutangamana na kuishi kwa pamoja.

Naye Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ametoa wito kwa wakenya kufuata nyayo za kristu kwa kutaa maovu ya dunia kama vile ufisadi miongoni mwa maswala mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *