Fanyeni kazi bila mapendeleo

Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima ametoa wito kwa mapadri na watumishi wote wa kanisa kutochagua eneo ambalo wangependa kuhudumu.

Akihubiri wakati wa hafla ya daraja ya Upadrisho katika dyosisi hiyo,askofu Kadima amesema kwamba wakristu katika pembe zote za ulimwengu wanakiu ya kujengwa kiimani na iwapo watumishi katika shamba la bwana watachagua italemaza utendakazi huo.

Wakati huo,askofu huyo amesisitiza haja ya makleri na majandokasisi kuwa na hulka ya kuungana mikono na wengine ili neno la mwenyezi mungu liweze kuenezwa kote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *