nafasi ya Meya kurejelewa

Viongozi wa dini ya kiislamu katika eneo la Kaskazini mwa bonde la ufa sasa wanashinikiza kurejeshwa kwa wadhifa wa Meya wa jiji kwenye mfumo wa serikali za utawala.

Wakirejelea ziara ya mfalme Chalrles watatu hivi majuzi humu nchini, viongozi hao wamesema kuwa mfalme huyo alikuwa anastahili kulakiwa katika miji mikuu na meya na wala sio rais kama ilivyoshuhudiwa.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa wahubiri wa dini ya Kiislamu katika ukanda huo Sheikh Abubakar Bini, viongozi hao wametoa wito kwa jopo linalohusisha serikali ya Kenya kwanza na muungano wa upinzani Azimio,  kuzingatia kurejeshwa kwa wadhifa huo katika miji mkuu nchini, kama njia moja ya kuboresha utoaji wa huduma zaidi kwenye miji hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *