Wakristu wameshauriwa kutii neno lake mwenyezi mungu ili wapate nafasi ya kuingia ufalme wa mbingu.
Kulingana na askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akizungumza katika kanisa la Mtakatifu Yosefu Chepkanga aliwataka wakristu kuwa tayari kila muda kulihubiri neno lake kristu kwa wale ambao hawamtambui mwenyezi mungu na kuwasaidia kuingia mbinguni.
Alisema ukristu wao utadhihirika watakapojitenga na maswala ambayo huenda ikawasongesha mbali na kristu kwa kutenda haki kwa wanyonge bila ya kuhujumu juhudi zao za kupata haki.
Aidha,askofu Kimengich aliwataka wakristu siku zote kuwa tayari kuishi na wengine kama ndugu na kutowatenga walio tofauti kisura maana wote wameumbwa kwa mfano wake kristu.