Kampuni ya usambazaji maji ya ELDOWAS kaunti ya Uasin Gishu imetangaza kukosekana kwa huduma ya usambazaji wa maji kuanzia kesho Jumatano saa tatu asubuhi hadi alhamis saa kumi na mbili jioni.
Kupitia notisi iliyotiwa sahihi na mkurugenzi wa kampuni ya eldowas peter biwott ameomba radhi kwa wakaazi akisema kuwa hali hii imechangiwa na marekebisho ambayo yatafanywa na kampauni hiyo katika vyanzo vya maji vya chebara.
Aliwaeleza wakaazi kuwa wakati marekebisho hayo yatakuwa yanaendelea sehemu ambazo hazijaathirika na ukarabati huu zitaendelea kupata usambazaji maji haya kama kawaida.
Wito umetolewa kwa wakaazi na sehemu ambazo zitaathirika kutafuta njia mbadala ya kupata maji sehemu hizi zikiwemo kimumu, university of eldoret,marakwet farm , maili nne, munyaka, kapsoya, action,, rift valley bottlers, elgon view, eldoret polytechnic,annex, langas, racecourse, ,chepkanga kapseret, marura, kamkunji, mwanzo, miongoni mwa zingine