Mwanamke mmoja ambaye amekuwa akiwalaghai watu wanaotafuta ajira mamilioni ya pesa katika ukanda wa North Rift baina ya Machi na Agosti mwaka huu atazuiliwa kwenye kituo cha polisi hadi Septemba 21 mwaka huu.
Akitoa uamuzi huo,hakimu mkuu wa mahakama ya Eldoret Dennis Mikoyan amesema mshukiwa huyo Dinah Jepchirchir atazuliwa kwa siku 14 kwenye kituo cha polisi cha Naiberi kuruhusu maafisa wa uchunguzi kukamilisha uchunguzi wao kabla yake kusomewa na kufunguliwa mashtaka dhidi yake.
Afisa wa uchunguzi Timothy Njuguna aliambia Mahakama kwamba mshukiwa huyo amewalaghai waaathiriwa wake kupitia kampuni yake ya Keter TravelS Group iliyoko mji wa Eldoret hii ni kutokana na ripoti waliyotoa zaidi ya waathiriwa 100 wakiahidiwa kupelekwa mataifa ya ugahibuni kwa kufanya kazi .
Mshukiwa alikamatwa katika eneo la Jua kali mnamo Agosti 3 mwaka huu ,huku upande wa uchunguzi ukiitaka mahakama kutumwachilia mshukiwa huyo kwani unasema mshukiwa huyo ako na stakabadhi hitajika kwa ushaidi tosha.
Hakimu mkuu akiruhusu mshukiwa kuzuiliwa kwa siku hizo 14 kabla ya kutoa maelekezo zaidi.