Wahudumu wa matatu katika kaunti ya Uasin Gishu wameeleza kuridhika kwao na shughuli za uchukuzi wakati huu wanafunzi wanaporejelea shuleni kwa muhula wa pili.
Wakizungumza mjini Eldoret,baadhi ya madereva wa magari ya umma walisema kwamba biashara imenoga sana hii leo ikizingatiwa idadi kubwa ya wanafunzi waliojitokeza kiasi cha raia wa kawaida kukosa magari ya usafiri.
Wahudumu hao wamesema kwamba japo hali ya maisha ni ngumu hawakuongeza nauli kwa sababu wanasema hali hii imewakumba wakenya wote.
Waliiomba serikali kuhakikisha inaangazia bei ya mafuta angalu mwananchi wa kawaida aweze kuwajengea biashara yao kwa kuabiri gari zao.
Aidha,baadhi ya wasafiri walilazimika kusubiri kwa masaa mengi kupata magari hasa za kuelekea Nairobi,Bungoma,Nakuru hata za kitale kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wanasafirishwa