Vijana wametakiwa kijitokeza na kujiendeleza kibiashara kwa njia ya kidijitali kama njia moja ya kijikimu kimaisha na kuinua uchumi wa taifa.
Mtandao wa kidijitali kwa sasa ni jukwaa ambalo linatoa nafasi nyingi za ajira kwa vijana, wengi wao walengwa na kampuni mbalimbali ili kunadi bidhaa zao.
Mkurugenzi wa Eldo Hub Magdalene Chepkemoi amejitosa katika taaluma hii ya kuwafunza vijana na kuwapa jukwaa la kijiendeleza kama anavyotueleza.
Miongoni mwa changamoto ambazo vijana hukabiliana nazo ni ukosefu wa pesa za kuanzisha biashara wengi wakikosa kujitosa katika ulingo wa biashra kutokana na hilo.
Ananuia kupanua jukwaa hili katika bara nzima ya Afrika na hata katika mataifa yaliyoka katika bara zingingine ili vijana waeze kutangamana na wenzao walio katika bara zingine.
Swali ni je iwapo vijana wananuia kujiunga na mtandao hii taratibu ni zipi?
Jukwaa hili lina wadau mbalimbali ambao kadhalika watafanikisha ndoto ya vijana ambao wananuia kufanya biashara kwa njia ya kidjitali.
Balozi wa marekani humu nchini Mac Whitmen anatoa wito kwa wakenya kufumka na kuingia katika majukwaa ya kidijitali badala ya kutumia mbinu na zamani, akihoji kwamba njia ya mtandao ndio suluhu la kipekee la kunadi bidhaa zao kwa njia rahisi na hata kuwapa nafasi ya kujiajiri.