Mmoja aachwa na majeraha ya mshale

Wenyeji katika kijiji cha Kapkitany eneo bunge la Aldai kaunti ya Nandi wanaishi kwa hofu baada ya kuvamiwa na watu waliowashambulia kwa mishale na kumwacha mtu mmoja na majeraha ya mishale huku nyumba tatu zikiteketezwa.

Akithibitisha haya mkuu wa polisi Nandi Kusini John Owouth amesema kwamba watu hao wametekeleza tukio hilo kwa kulipisha kisasi baada ya mwanamme mmoja kuwawa na pikipiki yake kuchukuliwa.

Alisema kwamba washukiwa watatu wamekamatwa akiwataka wakaazi kukumbatia amani.

Owouth aliwataka wenyeji wanapokuwa na tofauti zao watatue kwa njia ya amani huku akiwataka viongozi kuhakikisha wanawaelekeza vyema wenyeji kwa njia inayostahili.

Wakati huo wenyeji eneo hilo wanaitaka idara ya usalama kuwahakikishia usalama wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *