Wito umetolewa kwa wazazi kuwa karibu na wanao msimu huu wa likizo ndipo ndoto za watoto hao zikaja Wito umetolewa kwa wazazi kuwa karibu na wanao msimu huu wa likizo kwa kuwapa mwelekeo ili wasije wakijiingiza katika makundi ambayo yatawapotosha.
Kulingana na askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ni kwamba wazazi waendelee kuwalea wana wao inavyowapasa na kukoma kuwatelekeza maana hilo linaweza kuchangia watoto hao kuwa na hulka zisizo stahili na kuwaharibia maisha yao.wao inavyowapasa na kukoma kuwatelekeza maana hilo linaweza kuchangia watoto hao kuwa na hulka zisizo stahili na kuwaharibia maisha yao.
Askofu Kimengich aliwataka wazazi hao kuwa marafiki na walimu wa wana wao kila mara ndipo wafahamu kwa undani marafiki walio nao na kujitenga na wale wanaowaingiza kwa utumizi wa mihadarati.
Kadhalika,aliwataka wanajamii kuungana mikono kuwajengea maisha iliyobora watoto hao kupitia kanisa kuandaa mikutano za mafundisho na pia jamii kuwaelekeza vyema watoto hao kwa lengo la kuwajenga viongozi wanaohitajika wa miaka zijazo.