PUNGUZENI CHECHE ZA KISIASA

Ipo haja ya viongozi wa kisiasa nchini kukoma kutupa cheche za maneno ambayo huenda yakalemaza  mazungumzo ya maridhiano yanayoendelea hii leo baina ya mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja One Kenya.

Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,askofu wa dyosisi ya Eldoret Dominic Kimengich aliwataka wanasiasa kutoka mirengo zote za kisiasa kutoa nafasi kwa mazungumzo hayo na kukoma kuchochea akisema kwamba wanastahili kuepukana na ubinafsi na kuwa na uongozi wa kuigwa.

Alisema kwamba wanapoelekea kuzungumza wanapaswa kuepukana na misimamo mikali na kuwa na kauli moja ya kuelekeza wananchi na kwa manufaa ya wakenya akitaka mazungumzo hayo kuwa ya uwazi na ya kujenga na kuinua uchumi wa taifa hili.

yanajiri haya huku miungano ya Kenya Kwanza zikiendelea na mazungumzo yake wiki hii kuafikiana kuhusiana na matakwa mbalimbali kutoka kwa pande zote mbili mrengo wa Kenya kwanza ukitaka kufanyiwa mageuzi tume ya uchaguzi IEBC pamoja na maswala memngine huku Azimio ikitaka kuwekwa mikakati ya kupungzwa gharama ya maisha pamoja na kubatilishwa uidhinishaji wa sheria ya fedha mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *