Mahakama ya Eldoret iliambiwa kuwa aliyekuwa katibu wa muungano wa wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Uasin Gishu KCGWU akifanya kazi kama mtaalam wa afisa wa kliniki kwa muda wa miaka saba hajakuwa na cheti chochote cha kuruhusiwa kuhudumu kama afisa wa kliniki.
Naomi Arusei afisa msimamizi wa kliniki wa hospitali ya Pioneer viungani mwa mji wa Eldoret alikiri mahakamani kumruhusu Evans Makokah kuendelea kutoa huduma zake kama afisa wa afya licha ya kutokuwa na cheti cha kuhudumu kwenye nafasi hiyo.
Mbele ya hakimu mkaazi Barnabas Kiptoo alieleza mahakama kwamba licha ya kumshauri Makokah kuonyesha stakabadhi zake za masomo alikataa kumonyesha baada ya kuhamishiwa hospitali hiyo miaka minane iliyopita.
Alieleza mahakama kwamba kitengo hicho cha maabara kilikuwa chini ya usimamizi wa maafisa watatu wa afya Makokah akiwa ndiye pekee ambaye hakuwa na cheti husika akisema hakuweza kufahamu ni jinsi gani aliweza kuhakishiwa kitengo hicho bila stakabadhi husika.
Arusei alikua anatoa ushahidi wake kwenye kesi inayomwandama Makokha ambaye alifikishwa mahakamani kwa kuhudumu kwenye kitengo ambacho hana uchuzi kwalo na kukosa stakabadhi husika.
Mshukiwa huyo aaminika kuendelea kutoa huduma kuanzia Machi mosi 2001 na Agosti 25 2020 katika hospitali ya Pioneer kaunti ya Uasin Gishu akihudumu kama afisa msimamizi wa maabara na hakumiliki cheti chochote cha kitengo hicho.
Mshukiwa huyo alikamatwa na maafisa wa kitengo cha uchunguzi wa DCI mnamo Agosti 25 2021 ambapo alikua naazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Central na kufikishwa mahakamani kusomewa mashtaka dhidi yake.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Oktoba 2 ,2023.