Kuunganisha mkono uliokatwa kwa mara ya kwanza Mtrh

Hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi mjini Eldoret imepiga hatua kubwa katika uwanja wa matibabu baada ya kufaulu kuurudisha kwa kuupachika mkono uliokuwa umekatwa.

Mgonjwa aliyerudishiwa mkono huo alikuwa mhanga wa vita vya nyumbani ambapo alikatwa mkono.

Kulingana na taarifa ya hospitali hiyo ilisema kuwa mgonjwa huyo aliyetambuliwa kama mwenye umri wa miaka 35, alikatwa mkono wake wa kushoto kwenye kifundo cha mkono kufuatia shambulio la kinyumbani siku ya Jumanne.

Kisha alipewa rufaa kutoka Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Sigowet, Kericho, na kufika katika Idara ya Dharura ya MTRH saa 4 asubuhi na kiungo kilichotenganishwa kilihifadhiwa kwenye sanduku baridi.

Ndani ya dakika 15 alipelekwa kwenye ukumbi wa upasuaji ambapo timu mbili za wanachama 13 zilipishana kazi ya kuunganisha tena kiungo hicho na mchakato ulikamilika kwa ufanisi saa tisa alasiri.

Mgonjwa alihamishwa kutoka chumba cha wagonjwa hali mahututi ICU hadi Wodi ya Madaktari Mkuu wa Mifupa ambako ataendelea na ukaguzi na ukarabati wa kila siku.

Ikumbukwe kuwa Kenya ina madaktari bingwa watatu pekee wa upasuaji wa mikono, mmoja yuko Nairobi, mwingine Nakuru na Dk. Paul Mwangi kutoka MRTH.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *